Ajuza DJ Atumbuiza

Ajuza wa miaka 80 kutoka nchini Uholanzi, anarusha roho kila wakati kwa kuwatumbuiza zaidi ya watu elfu moja kwenye klabu moja  kila jumatatu usiku.

Ajuza huyo ni DJ na jina lake la kisanii anaitwa DJ Wika na pia huvalia mavazi ya kisasa pamoja na viatu vya juu al maarufu kama high heels huku akiwa na vidubwasha vya kuskizia muziki masikioni.

Kinyanya hicho huwasuta watu wanaomkashifu wakimtaka akae nyumbani na kulea  wajukuu,huku akielezea kuwa hakuna atakaye mfungia nyumbani kutokana na  umri na atarusha mroho kama anavyotaka mwenyewe.

Hata hivyo wadau wa burudani katika eneo analofanya kazi wameliambia shirika la Reuters kuwa  kazi yake  inaridhisha

 

Total Views: 25 ,