Achoki awarahadharisha wananchi

Kamishna wa kaunti ya Mombasa Evans Achoki amewataka wananchi kuwa makini wasiingie katika mtego wa matapeli wanaojifanya kuwa maafisa wa serikali wenye uwezo wa kuwapa idhini ya  kumiliki  bunduki kwa kiasi fulani cha fedha.

Akizungumza na wanahabari afisini mwake, Achoki amesema kuwa tayari baadhi ya wanasiasa na wafanyi biashara wametapeliwa zaidi ya shilingi elfu 50 kila mmoja na watu hao wanaojifanya maafisa wakuu wa polisi katika kaunti na  kutoka afisi ya kamishna huyo.

Achoki ameongeza kuwa kuna taratibu za kupata umiliki binafsi wa bunduki ,kutoka kwa serikali ambapo mtu anajiwasilisha kwa kituo chochote cha polisi,anajaza fomu na kisha kuandika barua ya maombi kupata bunduki hiyo.

Total Views: 230 ,