Ac Milan Wamnayatia Wilshere…..

Klabu cha Ac Milan nchini Italia kinapania kumsajili kiungo wa klabu cha arsenal Jack wilshere kutua ugani sansiro mwishoni mwa msimu huu…..
Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 26 mkataba wake unakamilika mwishoni mwa msimu huu na hayuko tayari kupunguziwa mshahara wake wa wiki kutoka £ 120,000 hadi £95,000 ili kusalia ugani Emirates…
Hatua hiyo imeifanya klabu ya Ac Milan kuanza kuafatia kwa karibu mchezo wa Muingereza huyo…
Huku hayo yakijiri mkufunzi wa arsenal profesa Arsene wenger amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini uingereza akilalamikia hatua ya mashabiki wa klabu hicho kusuia mechi kati ya Arsenal na Watford mechi ambayo walishinda 3-0.
Kwenye mechi hiyo ya jana licha ya Arsenal kuuza zaidi ya tiketi 59,131 za mechi hiyo kulishuhudiwa maelfu ya viti bila mashabiki.

Total Views: 145 ,