15 Kufikishwa kizambani kwa kosa la Kuchoma Shule

Wanafunzi takriban 15 waliokamatwa katika shule ya upili ya Nyakeyo kaunti ya Kisii wanatarajiwa kushitakiwa kwa makosa ya uchomaji leo Jumanne.

Hatua hii ni baada ya wanafunzi hao kuchoma nyumba mbili za familia wanaodai ilihusika na urogaji wa mwanafunzi mwenzao aliyeaga dunia wikendi iliyopita baada ya kuugua.

Kamanda wa polisi wa Kisii Hassan Abdi alithibitisha kukamatwa kwa wanafunzi kadhaa waliohusika na uchomaji wa nyumba hizo.

Wakati huo huo wanafunzi watano wa shule ya upili ya Chulaimbo Kisumu Magharibi walifikishwa katika mahakama ya Maseno  kwa kosa la uchomaji,ambapo waliachiliwa kwa dhamana ya shilingi elfu 30 na dhamana mbadala ya elfu mia 1 kila mmoja.

 Waziri wa elimu Amina Mohamed alisema kwamba wanafunzi watakaopatikana na makosa ya uchomaji wa shule hatawasajiliwa kwenye vyuo vikuu vya umma sawa na kunyimwa ufadhili huku vyeti vyao vya masomo vikiambatana na rekodi zao za uhalifu.

Total Views: 131 ,